Vidokezo
Ili kupata vituo vya basi vilivyo karibu, chagua Sehemu za Karibu kisha uchague Usafiri wa Umma.
Ikiwa unapanda basi lilelile mara nyingi, hifadhi vituo vyako kama alama. Weka beacon kwenye kituo unachoshukia, na Soundscape itakuambia kiko umbali gani ukiwa safarini.
Unaweza kuzima sauti ya beacon na bado usikie sehemu iko umbali gani. Soundscape inasema umbali mara kwa mara kadiri unavyosogea.
Ili kuichunguza sehemu kabla ya kwenda, fungua Taarifa za Mahali za sehemu hiyo na uchague Iga Mahali. Kisha Soundscape inafanya kazi kana kwamba uko huko.
Kwa maelekezo ya hatua kwa hatua, fungua Taarifa za Mahali za sehemu na uchague Fungua katika programu ya ramani. Soundscape inaendelea kufanya kazi huku programu nyingine ikitoa maelekezo.